Sunday, July 8, 2012

NI KUHUSU ZAIDI VIDEO PRODUCTION

Zaidi ni kwamba kampuni ya SULE'S INC. & ENTERTAINMENT Imeanza rasmi kufanya video za muziki hasa bongo fleva kwa wasanii wachanga. wote mnakribishwa.

Tuesday, June 7, 2011

MCHEZO WA NGUMI ILALA WAENDELEA KUHAMASISHA

Bondia Mohamed Matibwa wa Matimbwa Boxing akitupa konde bila ya mafanikio kwa Ibrahimu Class wa Amana Boxing 'Class' alishinda kwa K,O raundi ya nne wakati wa mpambano wa kuhamasisha mchezo wa ngumi mkoa wa Ilala uliofanyika katika ukumbi wa Panandi Panandi Ilala Bungoni.
Bondia Yakubu Abdulhamani (kulia) akirusha makonde kwa mpinzani wake Halili Hamisi wa Matimbwa wakati wa mchezo wa kuamasisha ngumi mkoa wa ilala Dar es salaam leo Hamisi alishinda kwa point. (Picha na Mpipicha Wetu)

Thursday, May 26, 2011

MAKING VIDEO YA KUDADADEKI YA MALFRED

Huyu nio Directo wa hii video kutoka OUTCOME
Directo Frank kutoka OUTCOME akifanya vitu vyake
Mpango mzima ulikuwa hivi! kwa habari zaidi gonga HAPA

VODACOM WAKABIDHI ZAWADI KWA WASHINDI WA LIGI KUU TANZANIA BARA

Mwakilishi wa timu ya Ruvu Shooting iimechaguliwa kuwa timu yenye nidhamu hivyo wamepata zawadi ya Mil.6.2
Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Salum Rupia akipokea mfano wa hundi yenye thamani ya sh.Mil. 42 iliyotolewa na wadhamini wa michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom ambao pia ndiyo washindi wa Ligi hiyo hafla hiyo ilifanyika katika Hoteli ya City Paradise leo mchana ambapo Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo Emmanuel Nchimbi ndiye alikuwa mgeni rasmi.
Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana U23 Jamhuri Kihwelu akipokea hundi yenye thani ya sh. Mil.17 ambapo timu yaSimba wamekuwa washindi w3a pili wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara .
Kutoka kulia ni Mtangazaji wa Redio One na ITV Maulid Kitenge, aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga Imani Mahugila Madega,Mhariri wa Habari za Michezo na Burudani Gazeti la Majira Suleiman Mbuguni na mwendeshaji wa Blog hii Khadija Kalili leo mchana katika hafla hiyo.

MAHAKAMA YAMWACHIA HURU MWAKALEBELA KUFUATIA KUISHINDA TAKUKURU

MAHAKAMA ya hakimu makazi mkoa wa Iringa kwa mara ya pili imemwachia huru aliyekuwa mshindi wa kura za maoni ndani ya chama cha mapinduzi (CCM) katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Frederick Mwakalebela na mkewe Celina baada ya kuonekana hawana kesi ya kujibu katika shitaka lililofunguliwa na taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) mkoa wa Iringa.

Mwakalebela na mkewe walifikishwa kwa mara ya pili mahakamani hapo na Takukuru baada ya kushinda kesi hiyo kwa mara ya kwanza miezi miwili iliyopita kabla ya Takukuru mkoa wa Iringa kuifungua upya kesi hiyo ya kuwakamata kwa mara ya pili watuhumiwa hao.
Hakimu wa mahakama hiyo Mary Senapee alisema kuwa mahakama hiyo inawaachia huru watuhumiwa hao kutokana na kutokuwa na kesi ya kujibu katika shitaka hilo la rushwa lililofunguliwa na Takukuru na kuitaka Takukuru kama haijaridhika kukata rufaa.
 Mwakalebela na mkewe walifikishwa mahakamani hapo na Takukuru kwa kosa la kutoa rushwa ya shilingi 100,000 kinyume na sheria ya kupambana na rushwa namba 11 ya mwaka 2007 kifungu cha 15(1)(b) kinachokwenda sambamba na sheria ya gharama za uchaguzi namba 6 ya mwaka mwaka 2010 kifungu namba 21 (1) (a) na kifungu cha 24(8).
Takukuru kupitia mwendesha mashtaka wake Imani Mizizi ilidai kuwa Juni 20, mwaka jana mshitakiwa Mwakalebela alidaiwa kutoa hongo ya sh. 100,000 kwa mwenyekiti wa kijiji cha Mkoga ,Hamis Luhanga ili awagawie wajumbe wa CCM 30 ambao waliitwa kwenye kikao hicho cha kujipanga kushinda kura za maoni CCM huku akitambua wazi kufanya hivyo ni kosa kwa habari zaidi ingia hapa

Thursday, May 19, 2011

TIMU YA TAIFA UNDER 17 NA 20 YAPATA KOCHA MPYA


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwajiri KimPoulsen, raia wa Denmark kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana wenye umri chiniya miaka 17 (Serengeti Boys) na chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kuanziaMei 15 mwaka huu.
Poulsen mwenye leseni ya kulipwa ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya(UEFA) katika ngazi ya diploma, na mkufunzi wa makocha wa kiwango cha juuanayetambuliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU) amesaini mkataba wamiaka miwili.Kabla ya kujiunga na TFF, Poulsen alikuwa kocha wa timu ya FC Hjorringinayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Denmark kuanzia Julai mwaka jana hadiMei Mosi mwaka huu. Mwaka 1989 alikuwa kocha bora wa mwaka nchini Denmark. Tuzo hiyo pia aliipatamwaka 2004 na 2005 nchini Singapore ambapo alikuwa kocha wa timu ya Taifa chiniya umri wa miaka 23.
Mwaka 2002 hadi 2003 alikuwa kocha wa timu ya Taifa yavijana chini ya miaka 18 ya Singapore. ya sifa za ukocha,
uteuzi wake pia umezingatia utaratibu wa TFF wa kuwa namakocha wenye falsafa moja ya mpira, hali ambayo inawajengea misingi mizuriwachezaji wa timu za vijana wanaopata fursa ya kuchezea timu ya wakubwa (TaifaStars). Utaratibu huo tuliuanzisha toka wakati wa Marcio Maximo akiinoa Stars ambapomakocha wa vijana nao walikuwa wakitoka Brazil.
Kocha wa sasa wa Taifa Stars,Jan Poulsen naye anatoka Denmark, na hana uhusiano wowote wa damu na Kim.
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF