Thursday, May 19, 2011

TIMU YA TAIFA UNDER 17 NA 20 YAPATA KOCHA MPYA


Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imemwajiri KimPoulsen, raia wa Denmark kuwa kocha wa timu za Taifa za vijana wenye umri chiniya miaka 17 (Serengeti Boys) na chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kuanziaMei 15 mwaka huu.
Poulsen mwenye leseni ya kulipwa ya ukocha ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya(UEFA) katika ngazi ya diploma, na mkufunzi wa makocha wa kiwango cha juuanayetambuliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Denmark (DBU) amesaini mkataba wamiaka miwili.Kabla ya kujiunga na TFF, Poulsen alikuwa kocha wa timu ya FC Hjorringinayoshiriki ligi daraja la kwanza nchini Denmark kuanzia Julai mwaka jana hadiMei Mosi mwaka huu. Mwaka 1989 alikuwa kocha bora wa mwaka nchini Denmark. Tuzo hiyo pia aliipatamwaka 2004 na 2005 nchini Singapore ambapo alikuwa kocha wa timu ya Taifa chiniya umri wa miaka 23.
Mwaka 2002 hadi 2003 alikuwa kocha wa timu ya Taifa yavijana chini ya miaka 18 ya Singapore. ya sifa za ukocha,
uteuzi wake pia umezingatia utaratibu wa TFF wa kuwa namakocha wenye falsafa moja ya mpira, hali ambayo inawajengea misingi mizuriwachezaji wa timu za vijana wanaopata fursa ya kuchezea timu ya wakubwa (TaifaStars). Utaratibu huo tuliuanzisha toka wakati wa Marcio Maximo akiinoa Stars ambapomakocha wa vijana nao walikuwa wakitoka Brazil.
Kocha wa sasa wa Taifa Stars,Jan Poulsen naye anatoka Denmark, na hana uhusiano wowote wa damu na Kim.
Boniface Wambura
Ofisa Habari TFF

No comments:

Post a Comment